Kutokana na makubaliano waloingia kati ya Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) na Taasisi ya Teknolojia ya Dar es Salaam(DIT) ya kuangalia fursa zilizopo kupitia TEHAMA na ni kwa jinsi gani zinaweza kutatua matatizo ya kijinsia ambayo yanaendelea hapa nchini kwa kukutanisha Jukwaa la Wasichana kwenye Vyuo vikuu (Youth Feminist Forum) ili kuzungumza changamoto wanazozipatia huko vyuoni.

Akizungumza wakati wa kufungua mafunzo hayo Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jinsia Tanzania Lilian Liundi amesema tuko hapa kuangalia changamoto na kwa namna gani wavhuo wa Taasisi ya DIT wanaweza kuleta suluhisho za hizo changamoto kupitia Teknolojia ili kurahisisha maisha kwenye jamii.

Amesema ikiwa kwa mfano kutatengenezwa mfumo wa kurahisisha kutoa taarifa za ukatili wa kijinsia matukio ya ukatili yatapungua kwasababu hatua za haraka zitachukuliwa na kupatiwa ufumbuzi.

“TGNP tunakuwa na watoto wa Shule za msingi ili kueleza vitu wanavyofanya nyumbani na wazazi wao hivyo kuwepo kwa suala la Teknolojia kwa watoto hao hasa katika kuripoti matukio mbalimbali ambapo mtoto anaweza kwenda kusema na huo mfumo kupeleka taarifa kwenye Mamlaka husika hivyo itasaidia kupunguza masuala ya ukatili wa kijinisia kwenye jamii inayowazunguka kwani watoto wengi ni waoga kuongea na wazazi wake”. Alisema Liundi

Naye Mhadhiri Mwandamizi kutoka Taasisi ya Teknolojia ya Dar es Salaam(DIT), Dkt. Asinta Manyele amesema leo tunaangalia ni kwa namna gani tunaweza kuitumia Teknolojia ili kutatua matatizo yetu yanayotuzunguka.

Pia ameipongeza TGNP kwa kuwa mwanga wa jamii kwani wanaangaza changamoto za jamii hasa ya kijinsia kwa kuyaweka wazi na kuyachukulia hatua hasa kuyapeleka kwenye mamlaka husika ambapo malengo makubwa ya Taasisi ya Teknolojia ya Dar es Salaam (DIT) ni kujaribu kutatua matatizo ya jamii kupitia teknolojia.
Mkurugenzi wa Mtandao wa Jinsia Tanzania Lilian Liundi akizungumza wakati wa kufungua semina ya Jukwaa la Wasichana kwenye Vyuo vikuu (Youth Feminist Forum) iliyokuwa na lengo la kujadili changamoto wanazozipata vyuoni pamoja na kuzitafutia utatuzi kupitia Teknolojia iliyofanyika katika ofisi za TGNP Mabibo jijini Dar es Salaam.
Mhadhiri Mwandamizi kutoka Taasisi ya Teknolojia ya Dar es Salaam(DIT), Dkt. Asinta Manyele akizungumza wakati wa semina ya Jukwaa la Wasichana kwenye Vyuo vikuu (Youth Feminist Forum) ili kujadili namna wanaweza kutatua changamoto wanazozipata vyuoni pamoja na kuzitafutia utatuzi kupitia Teknolojia.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Binti Makini na Mwezeshaji wa Semina hiyo Janeth John akiwasilisha mada zinazohusu Uongozi na Utawala kwa mtoto wa kike wakati wa semina ya Jukwaa la Wasichana kwenye Vyuo vikuu (Youth Feminist Forum) ili kujadili namna wanaweza kutatua changamoto wanazozipata vyuoni pamoja na kuzitafutia utatuzi kupitia Teknolojia.
Baadhi ya wanachuo kutoka vyuo mbalimbali wakifuatilia mada wakati wa semina ya Jukwaa la Wasichana kwenye Vyuo vikuu (Youth Feminist Forum) ili kujadili namna wanaweza kutatua changamoto wanazozipata vyuoni pamoja na kuzitafutia utatuzi kupitia Teknolojia.
Afisa Habari na Mawasiliano wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Monica John akitoa mrejesho wa wakati wa semina ya Jukwaa la Wasichana kwenye Vyuo vikuu (Youth Feminist Forum) ili kujadili namna wanaweza kutatua changamoto wanazozipata vyuoni pamoja na kuzitafutia utatuzi kupitia Teknolojia.

Picha za Pamoja

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...