Waumin wa Dini ya Kiislamu wametakiwa kuitunza misikiti na kuiweka katika hali ya unadhifu muda wote kwa maslahi ya vizazi vya Sasa na baadae.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Alhajj Hemed Suleiman Abdulla ametoa Kauli hiyo kwa niaba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Alhajj Dkt.Hussein Ali Mwinyi mara baada ya kuufungua Masjid RAHMAN uliopo Mfenesini Wilaya ya kaskazini "B" Mkoa wa Kaskazini Unguja sambamba na kujumuika na Waumini wa Msikiti huyo katika Ibada ya Sala ya Ijumaa.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar ametumia fursa hiyo kuwataka Waumini hao kuhuwisha na kuimarisha Mskiti hasa suala la usafi ili kuweka nidhamu kama Sheria ilivyoelekeza umuhimu wa suala la usafi katika Uislamu.

Alhajj Dkt Mwinyi ameeleza kuwa ni vyema kuandaa darasa kwa watoto na watu wazima kwa lengo la kuendeleza maadili mema na kuweza kupata ujira mbele ya Allah (S.W)

Amesema Mskiti ni Sehemu pekee inayotumika katika kutoa elimu ya Dini kwa vijana na wazee kuweza kumjua Mola wao na kuweza kufanya ibada kwa uhakika na kikamilifu pamoja na kujua sheria mbali mbali zilizomo ndani ya dini ya kiislamu.

Alhajj Hemed ametumia fursa hio kuwataka waumini na wananchi wa eneo Hilo kuendelea kutoa ushirikiano katika ujenzi wa madrasa pembeni mwa msikiti huo jambo ambalo litaweza kuwafunza vijana wa eneo Hilo na maeneo ya jirani kuweza kusoma na kufunza maadili mema.

Akimkaribisha Mgeni Rasmi Naibu Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Mahmoud Mussa Wadi amewataka wazazi kudumisha malezi kwa vijana wao ili kutekekeza wajibu wao kuipata taqwa kivitendo.

Amesema lazima wazazi na walezi kuwa na tahadhari juu ya malezi kwa Watoto ili kuwalea katika maadili mema na ukweza kupata ujira hapa duniani na kesho Akhera.

Akitoa Khutba ya Ijumaa Ustadh Salum kutoka Ofisi ya Mufti amewataka waumini kujitathmini na kujipanga kwa kuweza kuweka utaratibu wa kufanya ibada kwa wingi ili kupata fadhila za mwezi mtukufu wa Ramadhan.





Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Alhajj Hemed Suleiman Abdulla akifungua Msikiti kwa niaba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Alhajj Dkt.Hussein Ali Mwinyi uliopewa jina Masjid RAHMAN uliopo Mfenesini Wilaya ya kaskazini "B" Mkoa wa Kaskazini Unguja.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...