Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya mabadiliko madogo ya Baraza la Mawaziri kama ifuatavyo:

1. Amemteua Mhe. Jenista Joakim Mhagama (Mb) kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu). Mhe. Mhagama anachukua nafasi ya Mhe. George Boniface Simbachawene (Mb). Kabla ya uteuzi huo alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.


2. Amemteua Bw. George Boniface Simbachawene (Mb) kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora. Mhe. Simbachawene anachukua nafasi ya Mhe. Jenista J. Mhagama (Mb). Kabla ya uteuzi huo Mhe. Simbachawene alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu).

Uteuzi huu umeanza tarehe 01 Aprili, 2023.
Mawaziri wateule wataapishwa tarehe 02 Aprili, 2023 saa 3 asubuhi, Ikulu, Dar es Salaam.

Zuhura Yunus
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...