Na Muhidin Amri,Songea

WAKALA wa Barabara za vijijini na mijini(Tarura)mkoa wa Ruvuma,katika kipindi cha miaka miwili ya Serikali ya awamu ya sita ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan,umepokea jumla ya Sh. bilioni 43,924,114,171.33 kwa ajili ya matengenezo na ukarabati wa barabara.

Hayo yamesemwa na Meneja wa Tarura mkoani Ruvuma Wahabu Nyamzungu,wakati akitoa taarifa ya utekelezaji wa miundombinu ya Barabara zinazosimamiwa na Tarura katika kipindi cha miaka miwili ofisini kwake mjini Songea.

Nyamzungu alisema, fedha hizo zimeiwezesha Tarura kufanya matengenezo ya barabara kwa kiwango cha changarawe urefu wa kilomita 482.132,ujenzi wa barabara za lami kilomita 25.053,ujenzi wa madaraja 40 na ujenzi wa mifereji mita 3,400.

Alitaja miradi mingine iliyotekelezwa kupitia fedha hizo ni ujenzi wa barabara za zege katika maeneo yenye miinuko na miteremko kilomita 6.92 na kufungua barabara mpya kilomita 500.03 ambazo haijawahi kufunguliwa tangu tupate Uhuru.

Alieleza kuwa,katika kipindi hicho wamefanikiwa kupunguza kiwango cha barabara za udongo kutoka kilomita 6,159.19 hadi kilomita 5,658.41 na kuweka taa za barabarani 383 kati ya 340 za awali,na idadi hiyo inatarajia kuongezeka hadi kufikia 420 ifikapo mwezi Juni mwaka huu.

Asema,kuanzia mwaka wa fedha 2021/2022 serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan,imeongeza bajeti katika sekta ya miundombinu ya barabara kwa kutoa nyongeza ya fedha iliyotokana na za Tozo ya mafuta ya Petroli na Dizeli kiasi cha Sh.bilioni 7,000,000,000.

Nyamzungu alitaja fedha nyingine zilizotolewa ni kutoka mfuko mkuu wa serikali kupitia majimbo Sh.bilioni 4,500,000,000,fedha za mfuko wa barabara Sh.bilioni 7,383,070,020.89,fedha za mfuko wa maendeleo wa barabara Sh.bilioni 1,283,081,300.00 na kufanya bajeti ya mkoa huo kufikia Sh.bilioni 20,166,151,320.89.

Aidha alisema,kwa mwaka wa fedha 2022/2023 mkoa wa Ruvuma umepata nyongeza ya fedha itokanayo na Tozo ya mafuta ya petrol na dizeli Sh.bilioni 10,025,000,000 na fedha kutoka mfuko mkuu wa Serikali ( fedha za majimbo) Sh.bilioni 4,500,000,000.

Alisema,fedha kutoka mfuko wa barabara Sh.bilioni 6,918,627,877.44
na fedha za miradi ya maendeleo Sh. bilioni 1,390,000,000 hivyo kufanya bajeti ya mkoa huo kufikia Sh.bilioni 23,757,962,850.44.

Nyamzungu alieleza, baada ya nyongeza ya bajeti hiyo,miundombinu ya barabara imezidi kuimarika katika mkoa wa Ruvuma ambapo wamefanya matengenezo ya kilomita 1,372.581 za barabara kwa kiwango cha changarawe,kilomita 118.635 barabara za lami,kilomita 6.92 barabara za zege na kilomita 5,658 barabara za udongo.

Aliongeza kuwa,mtandao wa barabara wenye lami na changarawe hupitika kirahisi majira yote ya mwaka na mtandao wa barabara za udongo hupitika kwa shida wakati wa mvua.

Kwa mujibu wa Nyamzungu,kabla ya nyongeza ya bajeti iliyotokana na tozo ya mafuta pamoja na mfuko mkuu wa Serikali kwa fedha za majimbo, hali ya utekelezaji wa miradi ya barabara ilikuwa changamoto kubwa kutokana na serikali kuleta kiasi kidogo cha fedha kidogo.

Alisema,bajeti ya miradi kwa mwaka wa fedha 2020/2021 ilikuwa
Sh.bilioni 7,972,808,764.84,fedha za mfuko wa barabara kwa ajili ya kufanya matengenezo ya kawaida kilomita 549.61 ilikuwa Sh.milioni 1,355.98,matengenezo ya sehemu korofi kilomita 137.29 kwa Sh.milioni 1,164.83.

Kwa upande wa matengenezo ya muda maalum barabara zenye urefu wa kilomita 245.15 zimejengwa kwa Sh. milioni 3,559.58 na ujenzi wa madaraja madogo 4 Box kalavati 17 makalavati 11,madrifti 5 na mifereji mita 2,000 kwa gharama ya Sh.milioni 1,112.93.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...