Na Muhidin Amri,Madaba.

CHANGAMOTO ya upatikanaji wa mbegu bora za mahindi kwa wakulima wa mikoa ya Ruvuma na Njombe,linakwenda kumalizika na kuwa Historia baada ya kampuni ya Zambia Seed Co Ltd kuanza kuzalisha mbegu aina ZamSeed 638 katika shamba la Silverland Ndolela kata ya Mahanje Halmashauri ya Madaba mkoani Ruvuma.

Akizungumza na wadau wa kilimo katika siku ya maonyesho ya mbinu bora za kilimo Mkurugenzi Mkuu wa kampuni hiyo Frank Kileo amesema,kuanzia msimu wa kilimo 2023/2024 tatizo la upatikanaji wa mbegu linakwenda kuwa Historia kwa wakulima wa mikoa hiyo.

Alisema,mbegu za mahindi aina ya Zamseed 638 zitapatikana kwa wingi kwa mawakala katika wilaya zote za mkoa wa Ruvuma na Njombe,na kuwataka wakulima kutembea kifua mbele kwa kuwa sasa wana uhakika wa kupata mbegu bora na kwa bei nafuu.

Kileo alisema,kampuni ya Zambia Seed C Ltd iko tayari wakati wote kutoa majibu ya changamoto za wakulima kuhusu ubora,upatikanaji na bei ya mbegu ndiyo maana imeamua kusogeza huduma zake mkoani Ruvuma.

Kwa mujibu wa Kileo,katika msimu 2022/2023 kulikuwa na changamoto kubwa ya upatikanaji wa pembejeo hasa mbegu ambapo wafanyabiasahara walitumia nafasi hiyo kuuza mbegu kwa bei ya juu.

Alisema, hali iliyosababisha baadhi ya wakulima kushindwa kumudu gharama na wengine kukata tamaa na hata kutoendelea na shughuli zao za kilimo,lakini uzalishaji wa mbegu ya Zamseed 638 unakwenda kutatua changamoto zote zilizojitokeza katika msimu huu wa kilimo.

Alisema,kampuni ya Zambia Seed Co Ltd itaendelea kufanya tafiti mbalimbali wakati wote kwa kushirikiana na taasisi ya uthibiti wa ubora wa mbegu(TOSCI)ili kuhakikisha mbegu zinazozalishwa zinasajiliwa na kuwa na ubora ili kuongeza mavuno na kuwaondolea umaskini wakulima.

Kileo,amewashauri wakulima hapa nchini,kuanza kutumia mbegu zinazozalishwa na kampuni ya Zambia Seed Co Ltd ili kupata mavuno mengi,badala ya kutumia mbegu zinazozalishwa na makampuni mengine.

Amewaomba maafisa kilimo wa mikoa ya Ruvuma na Njombe na mikoa mbalimbali hapa nchini,kushirikiana na kampuni hiyo katika kuunga mkono juhudi za Rais Dkt Samia Suluhu Hassan katika mkakati wake wa kuwainua wakulima kutoka katika umaskini.

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Songea Wilman Ndile,amewataka wakulima kuzingatia kanuni za kilimo bora ili kupata tija katika shughuli zao za kilimo badala ya kuendelea na kilimo cha kizamani.

Alisema,kwa sasa kilimo ni biashara nzuri ambayo kama mkulima atafuata na kuzingatia kanuni za kilimo bora basi kuna uwezekano mkubwa wa kupata mafanikio makubwa.

Alisema,kwa kutambua mchango na umuhimu wa wakulima kama kundi lenye mchango mkubwa kiuchumi hapa nchini, serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan imeweka mfumo mzuri wa pembejeo za ruzuku zinazopatikana kwa bei nafuu.

Aidha Ndile,ameiomba kampuni hiyo kuuza mbegu zake kwa bei ndogo ili wakulima wengi waweze kumudu na kutumia katika shughuli zao za kilimo na hakuna sababu ya kuuzwa kwa bei kubwa kwa kuwa inazalishwa mkoani Ruvuma.

Mkuu wa wilaya,amewatahadharisha wakulima wa mikoa hiyo kuepuka kununua mbegu za mitaani zisizokuwa na ubora wala kuthibitishwa na serikali kwani kufanya hivyo kunaweza kupelekea kupata mavuno kidogo licha ya jitihada kubwa wanazofanya.

Baadhi ya wakulima, wameipongeza kampuni hiyo kuanza kuzalisha mbegu bora za mahindi ambazo zinakwenda kuongeza hamasa na kuchochea uzalishaji wa mazao mashambani.

Gelodian Millinga alisema,mafunzo hayo yatawasaidia wakulima kuongeza uzalishaji hasa kuanzia uandaaji wa shamba,upandaji na wakati wa kuweka mbolea.

Wilbroad Nyoni alisema, katika shughuli zao za kilimo changamoto kubwa ilikuwa upatikanaji wa mbegu bora kwani baadhi ya mawakala wasiokuwa waaminifu wanauza pembejeo zilizopita muda wa matumizi kutokana na tamaa ya fedha bila kujali upande wa wakulima.

Alisema,ujio wa kampuni hiyo na kuanza kuzalishwa kwa mbegu za mahindi aina ya Zamseed 638 katika mkoa wa Ruvuma,ni faraja kubwa kwa wakulima ambao sasa wana matumaini ya kupata pembejeo bora na bei nafuu.


Meneja masoko wa kampuni ya Zambia seed Co Ltd Jovinatus Fednand kulia,akiwasikiliza baadhi ya mawakala wa pembejeo kutoka wilaya ya Songea Rose Chale(Rose Minyungu kushoto) na Mary Christopher wakati wa maonyesho ya mbinu bora za kilimo yaliyoandaliwa na Zamseed Tanzania katika shamba la Kilimo Ndolela Halmashauri ya Madaba.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...