Baadhi ya mbegu za Nanasi zilizozalishwa kwa njia ya chupa zilizopo kwenye kituo cha Utafiti cha Kilimo TARI Mikocheni jijini Dar es Salaam.
Mtafiti wa Maabara ya uzalishaji mbegu za mazao kwa njia ya Chupa katika Taasisi utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI) mikocheni jijini Dar es laam,  Magreth Lupembe akizungumza na Michuzi Blog,  akielezea jinsi mimea iliyozalishwa kwa njia ya Chupa inavyokua vizuri ikiwa nje kwenye udongo wa kawaida. hapo akielezea mmea wa Mhogo.
Mashina ya Mkonge yanayoenda kuzalishwa mimea mingine ya mikongo katika maabara ya Mikocheni jijini Dar es laam katika Taasisi utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI).
Mtafiti wa Maabara ya uzalishaji mbegu za mazao kwa njia ya Chupa katika Taasisi utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI) mikocheni jijini Dar es Salaam, Magreth Lupembe akielezea hatua za mimea iliyozalishwa kwa njia ya Chupa kwenye maabara.


WAKULIMA wa mazao mbalimbali nchini wametakiwa kutumia mbegu pamoja na mimea iliyofanyiwa utafiti ilikuweza kufanya kilimo kwa faida ambapo kwa sasa serikali kupitia kwenye vituo vyake vya utafiti wameanza kuzalisha mbegu ikiwemo mbegu za mananasi na mkonge.

Akizungumza kuhusiana na suala hilo Mtafiti katika Maabara ya uzalishaji mbegu za mazao kwa njia ya Chupa katika Taasisi utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI) mikocheni jijini Dar es laam wakatia akizungumza na Michuzi Blog,  Magreth Lupembe amesema kuwa Wakulima na wakulima biashara waweze kutumia mbegu za mazao yaliyofanyiwa utafiti na taasisi hiyo ili kuongeza uzalishaji wa mazao.

Amesema kuwa uzalishaji wa miche hiyo unafanyika katika Kituo hicho  Serikali kupitia Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) inahakikisha kuwa teknolojia hiyo inasaidia taifa kukabiliana na uhaba wa mbegu bora za mazao.

Amesema mbegu hizo zote zinazalishwa kwa njia ya chupa ndani ya maabara hazina madhara yeyote kwa mtumiaji hivyo jamii itambue kuwa utafiti unaofanywa ni salama pia kwa mtumiaji.

"Teknolojia chupa maarufu kama 'Tissue Culture'   mmea huzalishwa ndani ya chupa iliyokuwa na virutubisho vyote vinavyosaidia mmea kukua kama unavyokuwa nje kwenye udongo wa kawaida.

Amesema kuwa TARI-Mikocheni inatakiwa kuzalisha miche ya Mkonge na Nanasi mingi zaidi ifikapo Julai mwaka huu ili kuwafikia wakulima katika mashamba darasa.

Amesema kituo hicho hakizalishi miche ya Mkonge pia huzalisha Nanasi, mbegu za mihogo zisizo na magonjwa na Viazi Vitamu kwa kutumia teknolojia ya hiyo chupa.

Magreth ameeleza kuwa uzalishaji wa mbegu bora kwa njia ya chupa ni tofauti na uzalishaji wa mbegu kwa njia zingine kama GMO kwahiyo muhimu jamii na wakulima kutambua kuwa nitofauti

Akizungumzia faida za uzalishaji wa mbegu hizo amesema kuwa inatunza vinasaba, mimea yote inafafana kwa kuwa itatoka katika shina moja lakini pia ladha ni ile ile na mbegu zake zinaweza kupandwa kama kawaida.

Faida nyingine ni kupunguza mahitaji ya mbegu kwa kutumia mbegu moja inatoa miche zaidi ya 200.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...