Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) umetoa mafunzo kuhusu mradi wa Boresha Habari katika Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TASUBA) ili kuhakikisha kwamba Waandishi chipukizi wa Vyuo vikuu na vyuo vya kati wanakuwa na uelewa hasa kwenye usawa wa kijinsia pamoja na uandaaji wa Bajeti yenye mlengo wa kijinsia wakati wa uandishi pamoja na kuripoti habari zenye mlengo wa kijinsia baada ya kuhitimu Masomo yao.

Akizungumza wakati wa kutoa mafunzo Mratibu wa Mradi wa Boresha Habari Mariam Oushoudada amesema lengo la mradi huo ni kuhakikisha wanafunzi wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TASUBA) wanapata elimu ya kutosha kuhusu masuala ya uandishi wa habari wa Kijinsia pamoja na kujua jamii kwa ukaribu zaidi hasa wanawake, vijana na Watu wenye ulemavu kabla hawajaanza kuripoti habari.

Amesema lengo ni kuweza kuwainua wanawake kwenye masuala yote ya uongozi pamoja na kujitambua kwani wanawake wengi bado hawana ujasili wa kuwawania nafasi kwani bado hawajapewa elimu ya kutosha hivyo mradi huu umekuja kwenye wakati mzuri hasa kwa wanachuo wa wanaosomea tasnia hiyo kwani watakuwa mabalozi wazuri.

Pia amesema Vyombo vya habari vingi haviripoti habari nyingi za masuala ya kijinsia hivyo kuamua kufanya mafunzo kwa wanahabari waliopo vyuoni itaweza kuleta hamasa na kutambua umuhimu wa habari zenye mlengo wa Kijinsia kwenye jamii inayowazunguka.

Naye Mwanafunzi wa TASUBA Rosemary Masusa amesema habari za masuala ya kijinsia wanazisikia mara chache hasa kwenye Uandishi hivyo kutokana na mafunzo hayo itawapelekea wanapokwenda kufanya kazi za Uandishi wa Habari wataweza kuzipa kiupaumbele kwani ndio ngao kwa jamii.
Mratibu wa Mradi wa Boresha Habari Mariam Oushoudada akitoa maelezo kuhusu mradi huo kwa wanafunzi wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TASUBA) waliofika kwenye mafunzo yaliyoandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania(TGNP) kwa kushiriikiana na chuo hicho kilichopo Bagamoyo mkoani Pwani.
Mratibu wa Vituo vya Taarifa na maarifa Jacqueline Mtesha akitoa maelezo kuhusu namna mtoto wa kike anavyoweza kijisimamia pamoja na kazi zinazofanywa na huo Jinsia Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) kwa baadhi ya wanachuo wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TASUBA) wakati wa mafunzo ya mradi wa Boresha habari yaliyofanyika katika katika ukumbi wa Chuo hicho Bagamoyo mkoani Pwani
Baadhi ya wanachuo wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TASUBA) waliofika kwenye mafunzo wakifuatilia mada zilizokuwa zinatole na watoa mada kutoka Mtandao wa Jinsia Tanzania(TGNP) hasa kwenye masuala ya kijinsia wakati wa mafunzo ya mradi wa Boresha Habari yaliyofanyika katika chuo hicho kilichopo Bagamoyo mkoani Pwani.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...