Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) imefanya operesheni maalum katika nyumba mbalimbali zilizopo katika kata ya Ununio ikiwa na lengo la kuwabaini wezi wakubwa wa maji wanaoikosesha Mamlaka mapato ya kutosha.

Akizungumza wakati wa operesheni maalum Meneja wa Mkoa wa Kihuduma DAWASA Tegeta, Victoria Masele amesema wamebaini mkazi mmoja wa mtaa wa Obama, kata ya Ununio (jina lake limehifadhiwa) alibainika kuhujumu miundombinu ya maji kinyume na sheria.

“Ukaguzi ni ili tuweze kuwabaini wale wote wanaohujumu miundo mbinu ya maji ambapo wanasababisha Mamlaka kushindwa kuendeleza miradi mingine na leo tumekuta mwananchi kajiunganishia Bomba lenye mita 300 linalopelekea watu wengine kutopata maji." Alisema Masele

Masele amesema uhujumu wa Miundo mbinu unasababisha upotevu wa pesa na kusababisha maeneo mengine isiyokuwa na mtandao wa maji kukosa huduma kutokana na baadhi ya wananchi kutokuwa waaminifu hivyo amewataka wananchi wenye matumizi makubwa ya maji kufikakatika ofisi za DAWASA kwa ajili ya kuomba kuunganishiwa maji yanayoendana na matumizi yao

Naye, Afisa Biashara kutoka DAWASA, Wendeline Komba amesema kuwa oparesheni hiyo itaendelea katika maeneo yote tunayotoa huduma na endapo tutawabaini basi hatua itakayochukuliwa ni pamoja na kuwafikisha Mahakamani kwani mteja huyu anatenda kosa kwa mara ya pili kwani mara ya kwanza alilipa faini ya shilingi milioni 40 baada  ya kukubali kosa lakini cha kushangaza amerudia kosa lilelile la kuchepusha maji tena.

Komba amesema sheria ya maji ya mwaka 2019 kupitia kifungu namba 5 inasema kuwa ni kosa kuchukua au kuchepusha maji kutoka kwenye miundombinu ya maji ambapo adhabu yake ni faini ya kiasi kisichopungua 500,000/= hadi 50,000,000/= au kifungo cha miezi 12 hadi miaka 5 au vyote kwa pamoja.

"Mwaka jana mteja huyu tulimkamata kwa wizi wa maji akalipa faini lakini tunashangaa tena kuunga bomba lingine ambalo liko kinyume na sheria na linazidi mita zinazotakiwa hivyo tumemkatia maji ili aweze kulipa faini zote na kama akishindwa tutamfungulia mashtaka kwa kuhujumu Miundombinu ya Mamlaka" alisema Komba  

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa mtaa wa Obama, Ndugu Julius Nhundulu ameipongeza Mamlaka kwa kufanya jitihada za kuwatambua wananchi wanaofanya hujuma na kusisitiza kuwa tabia hiyo iweze kuachwa mara moja na kufuata vigezo vya uhalali wa kupata huduma ya maji.
Meneja wa Mkoa wa Kihuduma DAWASA Tegeta, Victoria Masele( wa Pili kulia), Afisa Biashara - DAWASA Wendeline Komba (wa kwanza kulia), Mwenyekiti wa mtaa wa Baraka Obama, Kata ya Ununio Julius Nhundulu  wakishuhudia fundi wa DAWASA Jumanne Raymond alipokuwa anakata maji kwenye moja ya nyumba ambayo ilikuwa inaiba maji ya DAWASA. 
Meneja wa Mkoa wa Kihuduma DAWASA Tegeta, Victoria Masele( wa Pili kulia), Afisa Biashara - DAWASA Wendeline Komba (wa kwanza kulia), Mwenyekiti wa mtaa wa Baraka Obama, Kata ya Ununio Julius Nhundulu  wakishuhudia ukataji wa maji pamoja na kutoa miundombinu ya Mamlaka hiyo mara baada ya kugundua wizi wa maji kwenye moja ya nyumba mtaa wa Baraka Obama, Kata ya Ununio jijini Dar es Salaam.
Fundi wa Mkoa wa Kihuduma DAWASA Tegeta, Aron Libela akitoa bomba la maji kwenye eneo la Nyumba ya mkazi wa nyumba mtaa wa Baraka Obama, Kata ya Ununio jijini Dar es Salaam.
Mafundi wa DAWASA wakiendelea na kazi
Muonekano wa Mambomba ya maji mara baada ya kukatwa kwenye nyumba hiyo iliypopo mtaa wa Baraka Obama, Kata ya Ununio jijini Dar es Salaam.
Muonekano wa Mita mbili za maji alizokuwa ameunganishiwa na DAWASA kwa ajili ya matumizi yake kutolewa kwenye nyumba hiyo baada ya  kuchepusha maji kwa mara nyingine.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...