Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango amewasihi watanzania kutatua migogoro ndani ya familia kwa njia bora na sahihi zaidi ili kuepukana na athari zinazowakumba watoto ikiwemo kubaki yatima.

Makamu wa Rais ametoa wito huo leo tarehe 10 Juni 2023 mara baada kutembelea kituo cha watoto yatima cha Jerusalem Home of God’s Love ForChildren kinachohudumiwa na Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Mashariki na Pwani Usharika wa Kimara Jijini Dar es salaam. Kituo hicho kinahudumia watoto ambao hutelekezwa au kutupwa na wazazi wao kuanzia siku moja baada ya kuzaliwa kutoka maeneo mbalimbali ya nchi.

Amesema ni muhimu kila mtanzania kuguswa na kutambua ni kosa mbele ya Mwenyezi Mungu na jamii kutupa mtoto ambaye ni zawadi kutoka kwa Mungu. Ametoa wito wa familia kujiepusha na ugomvi na migorogoro na pale inapotokea basi yafaa kutumia njia bora za utatuzi kama vile dini, wazee na serikali.

Makamu wa Rais amezipongeza taasisi za dini nchini kwa kuendelea kujitoa kuhudumia watoto yatima na wale wanaopitia mazingira magumu. Aidha amewashukuru viongozi wa dini kwa kuendelea kuhubiri amani, kuombea viongozi wa nchi pamoja na kuliombea taifa.

Pia Makamu wa Rais ametoa shukrani za pekee kwa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Mashariki na Pwani Usharika wa Kimara Jijini Dar es salaam kwa fikra za kuhakikisha kituo hicho cha watoto yatima kinakuwa endelevu kwa kufanya uwekezaji mkubwa katika elimu na huduma za afya na kituo cha malezi kwa wazee.


Ameongeza kwamba suala la kuanzisha kituo cha huduma za afya pamoja na hospitali kwaajili ya kufundisha wataalamu wa afya katika eneo hilo litakuwa msaada kwa watoto yatima wanaolelewa hapo, jamii ya eneo hilo pamoja watanzania kwa ujumla. Amewapongeza kwa kupanda miti katika eneo la hekari zaidi ya 1500 kwa lengo la kuhifadhi mazingira

Halikadhalika Makamu wa Rais ametoa wito kwa watanzania kuacha tabia ya uvamizi katika maeneo ya taasisi za dini. Pia amesema ni muhimu kuhakikisha maeneo ya taasisi za dini yanapimwa mapema ili kuepusha migogoro inayoweza kujitokeza. Vilevile amewahimiza waumini na watanzania kwa ujumla kuona ni wajibu kutunza nchi kwa kupanda miti na usafi wa mazingira kwa faida ya vizazi vya sasa na vijavyo.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akiagana na watoto yatima wanaolelewa na Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Mashariki na Pwani Usharika wa Kimara wakati alipotembelea katika kituo hicho leo Tarehe 10 Juni 2023.



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango na Mkewe Mama Mbonimpaye Mpango wakiwa katika picha ya pamoja na watoto yatima wa kituo cha Jerusalem Home of God’s Love For Children kilichopo katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Mashariki na Pwani Usharika wa Kimara Jijini Dar es salaam wakati walipotembelea kituo hicho leo Tarehe 10 Juni 2023. (Kushoto kwa Makamu wa Rais ni Mchungaji Kiongozi wa Usharika huo Wibroad Matsai)



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akizungumza na wachungaji, walezi pamoja na watoto yatima wa kituo cha Jerusalem Home of God’s Love For Children kilichopo katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Mashariki na Pwani Usharika wa Kimara Jijini Dar es salaam. Tarehe 10 Juni 2023.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akimlisha keki mtoto Mercy Alex wakati alipotembelea kituo cha watoto yatima cha Jerusalem Home of God’s Love For Children kilichopo katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Mashariki na Pwani Usharika wa Kimara Jijini Dar es salaam. Tarehe 10 Juni 2023.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango na Mkewe Mama Mbonimpaye Mpango wakikata keki pamoja na watoto Mercy Alex na Baraka Bulenga wakati walipotembelea kituo cha watoto yatima cha Jerusalem Home of God’s Love For Children kilichopo katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Mashariki na Pwani Usharika wa Kimara Jijini Dar es salaam. Tarehe 10 Juni 2023.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akisikiliza maelezo kuhusu Kituo cha Kulea Watoto Yatima cha Jerusalem Home of God’s Love For Children kutoka kwa Mchungaji Wilbroad Matsai (wa kwanza kulia) wakati alipowasili Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Mashariki na Pwani Usharika wa Kimara Jijini Dar es salaam kuwatembelea Watoto yatima wanaolelewa na Kanisa hilo. Tarehe 10 Juni 2023.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango na Mkewe Mama Mbonimpaye Mpango wakiwasili katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Mashariki na Pwani Usharika wa Kimara Jijini Dar es salaam kuwatembelea watoto yatima wanaolelewa na Kanisa hilo katika kituo cha Jerusalem Home of God’s Love For Children. Tarehe 10 Juni 2023.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...