Na Mwandishi Wetu, Michuzi TV

WAFANYAKAZI zaidi ya 120 wa Benki ya Standard Chartered wameshiriki katika kufanya usafi kwenye ufukwe wa Bahari ya Hindi , lengo likiwa kupunguza taka za plastiki zinazotupwa baharini.

Wamefanya usafi huo eneo la bahari ya Kibo ikiwa ni sehemu ya kuelekea katika Siku ya Mazingira Duniani, ambayo itaadhimishwa Juni 5 ya kila mwaka chini ya kampeni yenye kaulimbiu ya #BeatPlasticPollution.

Akizungumza baada ya kufanyika kwa usafi huo, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered Tanzania Herman Kasekende, amesema mpango huo unalenga kupunguza kiasi cha taka za plastiki zilizotupwa baharini.

Ameongeza na ni utangulizi muhimu wa juhudi zinazoendelea za benki katika kusaidia na kuhamasisha utunzaji wa mazingira. Benki ya Standard Chartered inatambua umuhimu wa Siku ya Mazingira Duniani na imedhamiria kuendeleza utamaduni wa utunzaji wa mazingira ndani ya benki na jamii kwa ujumla.

"Mpango wa kusafisha ufukwe unaonyesha dhamira yetu ya dhati ya kutunza mazingira," alisema Herman Kasekende, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered Tanzania.

"Katika Benki ya Standard Chartered, siku zote tumekuwa tukiongozwa na adhama yetu ya kuwa na mifumo ya kibishara yenye uendelevu.Tunatambua kwamba mafanikio yetu yanahusiana sana na ustawi wa jamii ambazo tunafanya kazi.

"Kama taasisi ya kifedha, tuna fursa ya pekee ya kuleta athari chanya kwa kuwekeza katika suluhisho endelevu na kusaidia jitihada zinazokabiliana na changamoto za mazingira, " amesema.

Pia amesema Benki ya Standard Chartered inahakikisha kuwa inajumisha mbinu endelevu katika uendeshaji wake na kuwahimiza wafanyakazi wake kuwa mawakala wa mabadiliko. Kwa kujihusisha na shughuli zenye tija kama vile kusafisha ufukuwe wa bahari, benki inalenga kupunguza athari za uharibifu wa mazingira.

"Kwa miaka mingi, benki imetekeleza mipango kadhaa ya mazingira, ikiwa ni pamoja na uwekezaji mkubwa katika kufanya mapinduzi ya kibenki kwa kuleta huduma za kidijitali ili kupunguza kiwango cha kaboni, na kusababisha asilimia 90 ya miamala kufanywa kidijitali na kuondoa foleni katika matawi.

" Benki pia imeboresha udhibiti wa taka ,ikisababisha ongezeko la asilimia 360 katika taka zinazoweza kuchakatwa na kupungua kwa asilimia 40 katika jumla ya taka zinazozalishwa kila mwaka (tani 1.1 mwaka 2022), "amesema Kasekende na kuongeza mpaka sasa benki imepanda zaidi ya miti 3,000.

Pia amesema benki ya Standard Chartered itaendelea kutafuta njia bunifu katika shughuli zake za kibiashara na watajitahidi kubuni bidhaa na huduma za kifedha zinazounga mkono nishati mbadala, kuchochea uwekezaji wa kijani, na kukuza maendeleo endelevu.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered Tanzania Herman Kasekende akizungumza jambo mbele ya Wafanyakazi wa Benki hiyo,Wadau wa Mazingira pamoja na waandishi wa habari kuhusu utunzaji mazingira kuelekea Siku ya Mazingira Duniani

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered Tanzania Herman Kasekende sambamba na wafanyakazi wa benki hiyo wakishiriki kufanya usafi  eneo la bahari ya Kibo ikiwa ni sehemu ya kuelekea katika Siku ya Mazingira Duniani, ambayo huadhimishwa Juni 5 Juni ya kila mwaka chini ya kampeni yenye kaulimbiu ya #BeatPlasticPollution.


 


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...