Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe na Waziri wa Ufugaji na Uvuvi wakikata utepe kuashiria uzinduzi wa Ofisi itakayoshughulikia mabadiliko ya Kilimo Tanzania. Uzinduzi huo umefanyika kufuatia kongamano la Mifumo ya Chakula Afrika (AGRF) linaloendelea kufanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) kuanzia Septemba 05 hadi 08, 2023.

Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe na Kwa Upande wa Mkurugenzi Mtendaji, Mpango wa Mabadiliko ya Kilimo Afrika (AATI), Safia Boly wakizungumza kabla ya kuzindua ofisi ya ATO hapa nchini. Uzinduzi huo umefanyika kufuatia kongamano la Mifumo ya Chakula Afrika (AGRF) linaloendelea kufanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) kuanzia Septemba 05 hadi 08, 2023.
Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe na Waziri wa Ufugaji na Uvuvi akifungua pazia kwenye bango kwaajili ya uzinduzi wa Ofisi itakayoshughulikia mabadiliko ya Kilimo Tanzania. Uzinduzi huo umefanyika kufuatia kongamano la Mifumo ya Chakula Afrika (AGRF) linaloendelea kufanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) kuanzia Septemba 05 hadi 08, 2023.
Viongozi mbalimbali wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya uzinduzi ofisi ya ATO jijini Dar es Salaam.

Na Avila Kakingo, Michuzi Tv
WIZARA ya Kilimo kwa kushirikiana na Mpango wa Mabadiliko ya Kilimo ( African Agricultural Transfomation Initiative- AATI) wazindua ofisi ya Mabadiliko ya kilimo Tanzania, (ATO)

Uzinduzi huo umefanyika Septemba 05, 2023 jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano wa pembeni katika kongamano la Mifumo ya Chakula Afrika (AGRF) linaloendelea kufanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) kuanzia Septemba 05 hadi 08, 2023. 

Akizungumza  wakati wa uzinduzi wa ofisi hiyo, Waziri wa kilimo, Hussein Bashe amesema kuwa ofisi ya ATO itasaidia mabadiliko ya kilimo cha Tanzania na kuwa na sekta jumuishi, endelevu, na inayoendeshwa na ujuzi inayostahimili tabianchi. 

Amesema kuwa ATO itakuza mageuzi na ukuaji wa sekta ya kilimo nchini kupitia dira ya utekelezaji wa mikakati, kuongeza uwezo wa Serikali katika kutekeleza Mpango Kabambe wa Mabadiliko ya Kilimo, na kusaidia utekelezaji wa Mpango Kabambe wa Mabadiliko ya Kilimo kwa ufanisi na utekelezwaji wa kina. 

Pia Waziri Bashe amesema Ofisi pia itasaidia katika kujenga uwezo (ikiwa ni pamoja na uwezo na zana za kidijitali) na kupeleka zana za ufuatiliaji na tathmini katika maeneo ya husika.

Kwa Upande wa Mkurugenzi Mtendaji, Mpango wa Mabadiliko ya Kilimo Afrika (AATI), Safia Boly amesema  itaangalia sekta ya kilimo na ufugaji na uvuvi kwa kufuata kanuni na taratibu zilizotengenezwa kwa ajili ya kuendeleza juhudi za Serikali. 

akizungumza katika uzinduzi huo Waziri wa Ufugaji na Uvuvi, Abdallah Ulega amesema kazi kubwa ya Ofisi hiyoitakuwa ni kuangalia kanuni  iliyotengenezwa na Wizara kama inafatwa au haifatwi, pia lazima watoe taarifa ili waweze kumshauri Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Amesema ofisi hiyo itakuwa inafatilia na kuangalia wizara za kisekta kama zinatimiza wajibu kulinganisha na kanuni walizoziweka ili kufikia malengo yanyotarajiwa.

"Usipojitathmini kwa kazi unazozifanya unaweza kuona unafanya vizuri kumbe hauendi vizuri, kwahiyo ofisi ya ATO itakuwa inaangalia kazi za wizara za kisekta."

Akizungumzia ofisi hiyo ya ATO, Waziri wa Ufugaji na Uvuvi, Abdallah Ulega amesema kuwa ofisi hiyo ni kioo cha kuangalia utendaji kazi wa wizara za kisekta  hivyo wao wanawataalamu wa kila taaluma kwaajili ya kusaidia kujenga imani wadau wa maendeleo, wawekezaji wa kimataifa na mashirika mbalimbali. 

"Kwa sasa wanaofanya kazi na sisi na wanamichango yao ya kifedha, kuleta teknolojia walikuwa hawana kiunganisho na sisi sasa, walikuwa wanatuamini tuu,lakini wametengeneza chombo miongoni mwao ambacho kitawapa imani zaidi." Amesema Ulega


Tukio la uzinduzi limetoa elimu  kuhusu juhudi za Tanzania za kuharakisha mageuzi ya uchumi wake kupitia uimarishaji wa taasisi zake na ushirikiano na sekta binafsi, na kuboresha kubadilishana maarifa na kujifunza kuhusu changamoto, fursa na njia ya kusonga mbele kwenye mabadiliko ya kilimo.

Uzinduzi wa ofisi umeongozwa na waziri wa kilimo,  Mohammed Bashe, Waziri wa Kilimo, Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega,  na Mkurugenzi Mtendaji, Mpango wa Mabadiliko ya Kilimo Afrika (AATI), Safia Boly.

Katika hafla hiyo ya uzinduzi wa ofisi alikuwepo Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda, Tanzania, Omar Said, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Kazi, Uchumi na Uwekezaji, Zanzibar, Shaaban Mudrik Ramadhan Soraga, Waziri wa Uchumi wa Bluu na Uvuvi, Zanzibar, Suleiman Masoud Makame, Waziri wa Kilimo na Usalama wa Chakula, Sierra Leone, Henry Musa Kpaka, na washirika waanzilishi wa AATI, Obai Khalifa (Wakfu wa Bill na Melinda Gates), Dkt. Donal Brown (IFAD), Dkt. Agnes Kalibata kutoka Jukwaa la Chakula Afrika AGRA) na Omid Kassiri kutoka kampuni ya McKinsey.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...