THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.


Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

Archive for December 2008

HERI YA MWAKA MPYA WADAU WOTE


WATUKUFU WADAU WA GLOBU HII YA JAMII,
ASALAAM ALEIKHUM!
BWANA APEWE SIFA!
SHALOM!
WAAMA BAADA YA SALAMU, NAOMBA KWA IDHINI YENU, NA KWA KUWEKA TASWIRA HIYO YA DELTA YA MTO RUVU, NITOE SALAMU ZA UPENDO ZA HERI YA MWAKA MPYA KWENU NYIE WADAU WOTE POPOTE PALE MLIPO.
SEKUNDE, DAKIKA, SAA, SIKU, MAJUMA NA MIEZI IMEKATIKA KAMA MCHEZO VILE NA LEO TUNAUAGA 2008 NA TUKIJAALIWA MUDA MFUPI UJAO TUTAUANZA MWAKA 2009. NAWATAKIA MAISHA MEMA NA UTEKELEZAJI KWA VITENDO YALE YOTE AMBAYO WADAU MTANUIA KUYAFANYA MWAKA MPYA UJAO. KUMBUKA, YALIYOPITA SI NDWELE NA KUTELEZA SI KUANGUKA.
NI MENGI YAMEPITA, IKIWA NI YA FURAHA, HUZUNI NA KUCHEKESHA, BILA KUSAHAU UOSHAJI WA VINYWA, YOTE IKIWA NI KATIKA KUENDELEZA LIBENEKE LA GLOBU HII YA JAMII.
KAMA ALIVYO BINADAMU YEYOTE HAKUNA ALIYE KAMILI. KUNA WADAU AMBAO HAWAKURIDHIKA KWA HUDUMA ILIYOTOLEWA NA GLOBU YA JAMII, NA KUNA WALIORIDHIKA NA KUNA WALE AMBAO HAWAJALI, BORA SIKU IMEPITA NA AMEPATA JIPYA LA SIKU HIYO. NAMI DAIMA NAAMINI ULE USEMI WA 'KILICHO KIZURI KWA KUKU, NI KIBAYA KWA BATA MZINGA', HIVYO SIWEZI KUJIPA MOYO KWAMNA NINA UWEZO WA KURIDHISHA KILA MMOJA WA WADAU.
HIVYO NAOMBA RADHI PALE NILIPOTELEZA NA KWA UNYENYEKEVU MKUBWA WOTE NAWASHUKURU KWA USHIRIKIANO MKUBWA MLIOUONESHA NA AMBAO BADO MNAENDELEA KUONESHA.
NI HIVI MAJUZI TU GLOBU YA JAMII ILISHUHUDIA MDAU WA MILIONI 5 NA LEO TUNAKARIBIA HESABU YA MDAU WA MILIONI 5 NA ALFU 50, IKIONESHA NI JINSI GANI USHIRIKIANO HUO ULIVYO IMARA. NAWASHUKURU SANA KWA KUENDELEA KUTEMBELEA GLOBU HII PAMOJA NA KUCHANGIA.
MIAKA INAVYOKWENDA MBIO NI VIGUMU KUKUBALI KWAMBA SASA YAPATA MWAKA WA NNE NA USHEE TOKA GLOBU YA JAMII IZALIWE KULE HELSINKI, FINLAND, SIKU YA SEPTEMBA 8, 2005. ILIANZA KAMA GLOBU YA KUWEKA HEWANI KASHIKASHI ZANGU BINAFI LAKINI KADRI SIKU ZILIVYOZIDI KWENDA GEMU LIKAGEUKA, GLOBU IKAWA SIO YANGU TENA BALI NI YA JAMII NZIMA, NAMI NIMEBAKI TU KAMA MTUMISHI WA WADAU POPOTE DUNIANI, JUKUMU AMBALO NALITEKELEZA KWA FURAHA NA FAHARI.
NA WAKATI TUKIUAGA 2008 NA KUUKARIBISHA 2009 NAWEKA NADHIRI YA KUENDELEZA LIBENEKE KWA KADRI MOLA ATAVYONIJAALIA, HUKU NIKIENDELEA KUWEKA MASLHAI YA WADU MBELE KWA KILA JAMBO.
HERI NA FANAKA YA MWAKA MPYA WADAU WOTE!
-MICHUZI


Habari ja mchana Mh.Mchuzi,
kuna email nilipata toka kwa rafiki yangu karibu akanipa hii notice.pata kwenye attachment and happy new year to you the blog na wadau wote wa blog hii ya jamiizzzzz....
Mdau yban2


mdau wa tegeta alamba shangingi jipya la zain

Mkurugenzi Mkuu wa Zain Tanzania, Khaled Muhtadi akizungumza na waandishi wa habari wakati wa hafla ya kumpata mshindi wa gari aina ya Toyota Land Cruiser wa promosheni ya Endesha Ndoto Yako 2 ya Zain Tanzania, Msusa Jaffar wa Tegeta, jijini Dar es Salaam jana (Desemba 31, 2008). Kushoto ni mkaguzi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Bakari Maggid.


KAMPUNI ya simu za mkononi ya Zain Tanzania Limited leo imemchagua, Msusa Jaffar Msusa mwenye umri wa miaka 32, aliyebahatika kuibuka mshindi wa zawadi ya gari jipya aina la Toyota Land Cruiser jijini Dar es Salaam.

Msusa, mkazi wa Tegeta, Dar es Salaam ambaye ni fundi umeme, aliibuka mshindi katika bahati nasibu iliyochezeshwa Dar es Salaam leo kwenye hoteli ya Kilimanjaro Kempinski. Ameibuka mshindi wa zawadi kubwa kabisa kwenye promosheni ya Endesha Ndoto 2, akiwa ni mshindi wa 11 kunyakua gari, baada ya wengine 10 kuibuka na magari aina ya Toyota RAV 4 yaliyotolewa na Zain kuanzia Januari 2008.

Zain Tanzania ilitangaza kutoa jumla ya magari 11 katika promosheni yake kubwa kuliko zote ya Endesha Ndoto 2. Pamoja na magari hayo mapya kabisa Zain Tanzania pia imewawezesha wateja wake kujishindia muda wa maongezi na fedha taslimu na kwa wale ambao waliweza kujikusanyia pointi, pia wameweza kushinda simu, ipod na zawadi nyingine nyingi.

“Kama mnavyofahamu Zain Tanzania imekuwa ikiendeleza jitihada zake za kubadilisha maisha ya wateja wake kwa kuwazawadia magari mapya kutoka Toyota Tanzania yakiwa yamesajiliwa kwa jina la mshindi na kulipiwa ushuru na bima zote husika.

“Promosheni ya Endesha Ndoto 2 ya Zain kwa mwaka 2008 imefikia tamati leo, tumekabidhi magari 11 mapya kwa Watanzania waliobahatika kuingia na kujishindia zawadi mbalimbali likiwemo gari jipya la kifahari aina ya Toyota Land Cruizer.

Leo tumemchagua mshindi wa 11 aliyejinyakulia gari hilo la kifahari,” alisema Khaled Muhtadi, Mkurugenzi Mkuu wa Zain Tanzania.


kilima nanihii...

wadau wengi wameomba taswira hii ya kilima nanihii pale masake, dar, ili kuaga mwaka kwa kumbukumbu za uroda wa sehemu hiyo. nawasilisha...


mchezo wa chess kuagia mwaka mkahawa wa vitabu

Mheshimiwa balozi wa nanihiiiii…..
Leo tunafunga mwaka wa 2008 na mchezo wa chess katika mkahawa wa vitabu wa SOMA. Wadau wote ambao wapo Dar es salaam wanaweza kuja kucheza au kusomeshwa jinsi ya kucheza gamu la chess.
Wooote mnakaribishwa
Manager wa Mkahawa
Godfrey George Kioko


Mada ya kupunguza Stress!

Wengine huku ughaibuni at 1200hrs / 12.00noon unakuta ni giza totoro! Je, hapa nitaita mchana au usiku?

Mtazamo mwengine: Majira ya Usiku na Mchana yanatokana na kiasi cha mwanga au muda katika saa?
Naomba maoni yenu!
Mdau Ughaibuni


sherehe ya pamoja baada ya nondozzz

wadau wakisherehekea kwa pamoja baada ya kula nondozzz chuo cha uhasibu, kurasini, dar. chini ni keki maalumu iliyoandaliwa kwa sherehe hiyo ilofanyika ukumbi wa kizota, sabasaba.
mkeka mpya kwa barabara ya mandela rodi

barabara ya mandela rodi yenye umri wa zaidi ya mwongo mmoja ikipigwa mkeka mpya


kausafiri ka mdau ben kinyaia

mtangazaji wa eatv ben kinyaia akikatiza mitaani na kausafiri kake.


mdau wa usa river akomba milioni moja ya zain

Mfanyakazi wa Zain Tanzania, Blandina Billy, akibonyeza kitufe kwenye kompyuta kumpata mshindi wa tisa wa sh. milioni 1 wa promosheni ya Endesha Ndoto Yako 2 ya Zain Tanzania, Mussa Ramadhani wa Usa River, Arusha, jijini Dar jana. Shoto ni mkaguzi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Humudi Abdulhussein, Meneja (Kitengo cha Masoko) wa Zain Tanzania, Ellen Lupili na kulia ni Ofisa Mawasiliano ya Ndani wa Zain Tanzania, Dangio Kaniki.


RAIDA HIGH SCHOOL

KWA HABARI ZAIDI WASILIANA NA:
+255 784 418 788
+255 222 807 605
+255 786 122 471
+255 754 824 723
+255 784 418 788
Fax: +255 222 807 605
PROF. RUTH MEENA
CEO
RAIDA HIGH SCHOOL AND LEARNING CENTRE


AfrikaNite New Year's Eve bash in Beijing, China


Hello everyone!

Africans living in Beijing and near provinces are invited to the New Year Eve bash 31.12.2008 @ Pilipili!!

From 10:30pm Till late.

Dress code: Black & White.

Infoline 13717640747

ONE LOVE~~~~!


HAPPY NEW YEAR TO ALL TANZANIANS AND AFRICANS ALL OVER THE WORLD.


SALAMU TOKA KIJITONYAMA CHIPUKIZI S.C

Kikosi cha kwanza KCSC
Kikosi cha pili KCSC
Uongozi na Wachezaji wa Kijitonyama Chipukizi Sports Centre unatoa shukurani kwa wadau wote wa michezo hususani mpira wa miguu kwa misaada ya hali na mali waliyotupatia katika mwaka huu wa 2008 unaomalizika leo.
Tunapenda kuwataja wafuatao:-
Wakazi wa Kijitonyama,Uongozi wa Shule ya Msingi Kijitonyama,Uongozi wa Kata ya Kijitonyama,Uongozi wa Kifa,Uongozi wa Kidiyosa, Mh.Iddi Azzan Mbunge wa Kinondoni, Mwenyekiti serikali ya mtaa Bwawani, na Balozi Issa Michuzi(blogu ya jamii).
Wengine ni Bw. Prince Tumaini wa Bongosoccer,Bw F.Mressa wa CRDB, Sheikh Issa Kamtande,bw,J.Makongo(Mlezi wa KCSC). Bw Esmail Mwenda Mwenyekiti wa CCM Vijana Kata ya Kijitonyama, Bw Hussein Sapi,Bw Kaijage waTanzania soccer academy, Uongozi wa Mwiba F.C .

MAFANIKIO YA KCSC KWA MWAKA 2008.
Timu A(U-17) imetwaa mataji mawili yaani Kombe la Sinza 2008,Kombe La Upendo Na hatua ya nusu fainali kombe la Copa CocaCola Ngazi ya Wilaya.Hatua Nusu Fainali Kombe La Pasaka.
Timu B (U-14)Ubingwa wa Kombe La Idd 2008
MALENGO YA KCSC KWA MWAKA 2009.
Kijitonyama Chipukizi tunatarajia kushiriki ligi mbalimbali mpira wa miguu ngazi ya kata na wilaya kwa timu zote mbili yaani timu A na Timu B na ifikapo mwezi wa Oktoba, Timu A itaingia kwa mara ya kwanza katika ligi ya TFF ikiwa na lengo la kuuza wachezaji kwa timu kubwa, kuendelea kutafuta wadhamini mbalimbali wa vifaa vya michezo.

Pia kutafuta wadhamini watakaotudhamini katika ushiriki wa ligi mbalimbali tulizozitaja hasa kwa mfano gharama za ,chakula,maji ya kunywa,usafiri wa kwenda na kurudi katika mechi,posho za wachezaji na viongozi N.k .

Kuwa karibu na Timu kubwa kwa kucheza mechi za Kirafiki na timu zao za kikosi cha pili na kupata ushauri mbali utakaotolewa na Walimu wa timu hizo.
Kuwa na mawasiliano ya moja kwa moja na wakala wanaotafuta wachezaji ndani na nje ya nchi.
Ni matarajio yetu kuwa mtazidi kutuunga mkono katika kukuza vipaji
Tunawatakia kila la Heri ya Mwaka Mpya wa 2009
CHRIS FIDELIS
kny KCSCmsaada tutani

Habari na pole na kazi,naomba msaada natafuta website ya NATIONAL BOARD FOR MATERIALS MANAGEMENT (NBMM)kama kuna mtu yeyote anaifahamu maana iliyokua inatumika mwanzo ni kama imepotelea hewani,naomba mnisaidie
asante,
anna
---------------------------------------------------------
Hi...
I am trying to get in touch with the following person: Ester Mkomwa. If anybody knows her contacts, please get in touch with me. Thanks. You could also ask her to contact me via email:
Thanks.
Joe


VODACOM - TALK FOR LESS EVERYDAY!!

Vodacom Tanzania always keeps you CONNECTED while enjoying VALUE FOR YOUR MONEY as you communicate with your friends, family and loved ones in the year 2009!!

1. Chombeza Time: Talk for HALF A SHILLING per second everyday! Enjoy late night calls with your loved ones everyday! Sweet talk your loved ones everyday for HALF A SHILLING per second (Taxes excluded – VAT & Excise) from 10pm to 6am everyday.Available on Vodacom to Vodacom calls only.
*Terms & Conditions apply.

2. VodaJamaa: Talk to your TWO favourite Vodacom numbers for ONE SHILLING per second everyday! Wish your TWO loved ones NEW YEAR in style! Vodacom customers can call their TWO favourite Vodacom numbers and talk for only ONE SHILLING (Taxes excluded – VAT & Excise) from 6am to 10pm everyday for 30 days.

To register, customers should follow the below steps;

First step: To register, dial *144*01* Vodacom first number*Vodacom second number#


Second step: To confirm, dial *144*02#Third step (Optional):

If you have made an error while setting up your VodaJamaa, then you can cancel by dialling *144*03#

NOTE: To check up your VodaJamaa settings and to know the next day you can change your TWO favourite Vodacom numbers, dial *144# *
Terms & Conditions apply.

3. Vodazone: Talk for as low as HALF A SHILLING per second everyday! With Vodazone, Vodacom prepaid & VodaJaza customers can make Vodacom to Vodacom calls and talk for as low as HALF A SHILLING per second (Taxes excluded – VAT & Excise) from 6am to 10pm everyday.

The rate you pay is based on the location and time of the day. Customers who wish to view Vodazone rates can follow the below steps:

1. Go to Main Menu

2. Then press settings

3. Then press network

4. Then set ‘Cell Info Display ON’


Fore more information,

call FREE 0763 300011

(Swahili) or 0763 300012

(English)

*Terms & Conditions apply.


atc yafunguliwa mbawa zake

baada ya kufungiwa siku kadhaa kupaa angani, hatimaye shirika la ndege la atc limepewa tena leseni na kufunguliwa mbawa zake leo. ila wafanyakazi wake bado wako hoi bin taaban kwa kukosa mshiko wa mwezi desemba ambapo krisimasi hii waliishia kuula wa chuya. soma zaidi habari hii kwa kubofya hapa kwa ung'eng'e ama bofya hapa kwa kimatumbi


mdau dennis londa wa helsinki ndani ya nyumba

leo nimebahatika kugongana na mmoja wa wadau waandamizi wa globu ya jamii, dennis londa, anayepiga kitabu na boxi huko helsinki, finland.
Mdau Dennis alikuwa vekesheni bongo na mchana huu kapaa kurejea ughaibuni kuendeleza libeneke.
Huyu mdau pamoja na fide mtimkubwa walikuwa mashuhuda wakati globu ya jamii ilipokuwa leba ikizaliwa huko helsinki septemba 8, 2005 (bofya hapa) , chini ya maelekezo ya mkuu wa wadau, mkombozi na mwanzilishi wa globu za kiswahili kaka ndesanjo macha (bofya na hapa). Wote hawa pamoja na wengine kibao nawashukuru kwa ushauri wanaonipa katika kuendeleza libeneke. Ndesanjo, Mtimkubwa, Dennis Mbarikiwe!
nyuma yetu ni club billicanas ambayo baada ya ukarabati na ukarafati wa takriban mwaka mmoja, sasa iko katika hatua za nchani kabla ya kufunguliwa rasmi. redio mbao zimesema ilikuwa ifunguliwe kesho lakini hatua hiyo imesitishwa kwa sababu ambazo hazijaelezwa na kwamba sasa itafunguliwa januari 8, 2009.


mdau asimulia kisa cha madawa ya majaribio...

Habari ya kazi bro Michu?
Naomba utoe kisa hiki, ila sina nia mabaya na Mtu yoyote. natoa kisa cha kweli kilichonitokea mimi.
Kuna kipindi niliumwa malaria sana nikaenda Hospital fulani kubwa (private hospital)sitaitaja jina kwa sasa ila mkitaka niwapa jina baadaye., sasa nikaenda hospitalini hapo ilikutibiwa nikaulizwa unataka tukuchome sindano au tukupe vidonge, nikachagua nipewe dozi ya vidonge, nilichagua sio kwa kubana matumizi wala nini ila kampuni ilikuwa inalipia matibabu kwa wafanyakazi wake kwa gharama yoyote.
Sasa nikapewa vidonge hivyo nikaenda navyo nyumbani kwenda kutumia, kilichotokea baadaya ya kama dk 40 mdomo ukaanza kubana na kisha sehemu ya chini kwenda upande kwa nguvu na kisha kuacha kidogo na kisha kurudia rudia rudia, wewe...nilipiga kelele nikamwambia mdogo wangu aendeshe gari langu anipeleke kurudi hospitalini hapo.
Tulipofika akasimulia yalonikuta na tukaonyesha dawa tulizopewa. Chap chap nikachomwa sindano ya kukata makali ya dawa hiyo na mdomo ukatulia, na ulipotulia nikauliza je kwa nini mlinipa dawa hii, wakasema sorry hii dawa ilikuwa kwenye majaribio inatoka India, na ina allergy kwa watu wengi. Sorry tutakupa ingine.
Nikachanganyikiwa kidogo. Nikasema it's enough. Ngoja nikajaribu hospitali ingine. Nikaenda huko kwingine ndio nikapata tiba ya vidonge vinavyofahamika.
Sasa je kwa namna hiyo je tutafika kweli, na hospitali hiyo kubwa sasa majaribio ya nini tena wakati kampuni kubwa zinagharamia kwa gharama kubwa matibabu kwa wafanyakazi wake ?
Na Hospitali hiyo inatumia dawa ambayo hata jina lenyewe huwezi kulipata kirahisi kwenye Pharmacy za mitaani mje kujaribia kwa wagonjwa wanaokuja hapo? hiyo inakuwa sio vizuri kwani mnaweza kuua watu wengine au kupoteza biashara naomba kuwasilisha kwa wale wenye Hospitali jaribu kujali maisha ya watu tumieni madawa yanajulikana na yaliyopitishwa kwenye viwango vya ubora.
Kama mnaona Gharama ni kubwa kwa Madawa hayo ni Bora Mkaomba serikali iangalie kwa makini swala hilo.
Asante
Mdau E.K


raida high school yakukaribisha ujiandae kula nondozzz

For more information contact the school at:
+255 786 122 471,
+255 754 824 723,
+255 784 418 788,
+255 222 807 605,
Fax +255 222 807 605
PROF. RUTH MEENA
CEO
RAIDA HIGH SCHOOL & LEARNING CENTRE


ticha chiwalala atunukiwa tuzo ya muziki ufini

Arnold Chiwalala mwanamuziki/mwalimu wa Kitanzania (katikati, akiwa na watunukwa wenzie) anayechukua Shahada ya Uzamivu katika Chuo Kikuu Cha Muziki Cha Sibelius (Sibelius Academy) ametunukiwa Tuzo ya Dhahabu ya muziki wa Ala ya Kantele 2008. Kantele ni ala ya kiasili ya Finland.
Tuzo hii hutolewa kila mwaka na Wizara ya Utamaduni ya Finland kwa mwanamuziki bora ambaye amechangia katika utunzi(composition) na uendelezaji (promotion) wa ala ya Kantele ndani na nje ya Finland.

Arnold Chiwalala ni muhitimu na mwalimu kutokea Chuo cha Sanaa Bagamoyo. Vile vile ni mwanamuziki, mtunzi, muandishi wa nyimbo na mbunifu wa miondoko (choreographer).
Kazi za Mwalimu Chiwalala zinatambulika kimataifa ambapo ameshiriki katika warsha, matamasha na makongamano sehemu mbali mbali ulimwenguni ikiwemo Tanzania, Zambia, Zimbabwe, Msumbiji, Uingereza, Ujerumani, Marekani, Urusi, Norway, Denmark,Sweden,Finland, Estonia na Yugoslavia.
Mpe pongezi Arnold Chiwalala kupitia email:
ama Simu
+358405290622
tuzo aliyopewa Arnold Chiwalala


Asia ashinda tuzo ya mbunifu bora wa mavazi bongo, ajiandaa na Lady in Red 2009

mama wa mitindo asia idarous akikabidhiwa tuzo ya mbunifu bora wa mavazi bongo na mkurugenzi wa kampuni ya smiling faces, Auntie carolyne, kwenye onesho la Red Carpet katika hoteli ya Regecy Park hotel ya Mikocheni, Dar. Asia alishinda baada ya wadau kutoa maoni yao kupitia kituo cha DTV ambapo alishindanishwa na baadhi ya wabunifu wakubwa nchini
supa modo belina akionesha moja ya mavazi mapya kibao yanayobuniwa na mama wa mitindo asia idarous. hili gauni la jioni ni mojawapo ya mikwaju itayooneshwa kwenye shoo kabambe ya kila mwaka ya Lady in Red inayofanyika hoteli ya Kempinski Februari 6, 2009.Zeyana Seif wa BBC afariki dunia

hayati Zeyana Seif akipozi na wafanyakazi wenzie wa BBC London enzi za uhai wake. Picha ni kwa hisani ya BBCSwahili.com

Imeandikwa na Mwandishi wa BBC

Zeyana Seif, mwanamke wa kwanza kabisa kusoma habari kwenye redio, katika BBC, hatunaye tena. Amefariki ghafla jana huko London.

Mkuu wa Idhaa ya Kiswahili, Solomon Mugera kwa niaba ya shirika la Utangazaji la Uingereza BBC ametoa pole kwa ndugu na jamaa za marehemu.

Akimzungumzia marehemu, Bw. Solomon amesema alikuwa mcheshi na mchangamfu, na daima alikuwa tarari kutoa msaada wowote katika fani ya utangazaji.
Alistaafu mwaka 2005.

Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema
-----------------------------------------------------------------------------
GLOBU YA JAMII INATOA POLE KWA FAMILIA YA MAREHEMU PAMOJA NA WADAU WOTE WA BBC CHINI YA UONGOZI SHUPAVU WA BW. SOLOMON MUGERA. MOLA AIWEKE ROHO YAKE MAHALI PEMA PEPONI.
-MICHUZI


BASH LAFANA JIJINI ROME

DJ BEKA akifanya vitu vyake ndani ya African Bash mjini Rome ,iliyofanyika tarehe 26/12/2008 ambayo ilifana sana.Wadau wanatoa pongezi kwa matayarisho mazuri na muziki wa kizazi kipya uliopagawisha ndani Rome mpaka kusheee...!!

Kwa picha zaidi tembelea:


da'mwantumu la nondozzz ukerewe

DA' MWANTUM KITWANA DAU ANAPOZI BAADA YA KUVUTA NONDOZZZ ZA ACCOUNTING AND FINANCE TOKA CHUO KIKUU CHA UNIVERSITY OF EAST LONDON (UEL) NONDOZ ZA ACCOUNTING AND FINANCE.

GLOBU YA JAMII INATOA HONGERA KWA MDAU MWANTUMU KWA KULA NONDOZZZ


njenje kuuaga 2008 na kuukaribisha 2009 karimjee hall

kama kawaida yao Kilimanjaro Band maarufu kama Wana-Njenje (pichani) watauaga mwaka 2008 na kuukaribisha 2009 pale pale pa kawaida yao, yaani viwanja vya karimjee hall jijini Dar KESHO JUMATANO kuanzia saa tatu unusu usiku hadi kokoliko.

kiongozi wa njenje, waziri ally, kaiambia globu ya jamii sasa hivi kwa ung'eng'e kwamba wao huwa hawa tale advantage ya sikukuu kwa kupandisha kiingilio na kwamba dau lao mlangoni ni lile lile la miaka nenda miaka rudi la kiasi cha mboga yaani sh. 5,000/- tu!

waziri kasema pamoja na burudani kibao na kuduarika pia kutakuwa na big screen ambayo itachezwa dvd za njenje tokea miaka ya 80 na pia atayependa atauziwa. ila kasema ziko chache kwa hiyo mdau ukifika tu toa oda.


kp leoujumbe na taswira toka kwa mdau wa kigali

Habari za leo wadau, 'Amakuru yuno munsi'
Mh.Balozi wa Zain mtandao usiopatikana huku Rwanda (Kigali) na mkuu wa wilaya ya nani hii. Najua kipindi kile ulikua huku ulitunyima baadhi ya taswira muhimu ambazo watanzania wanazijua ila tu kwa wale wapenzi wa sinema.

Nakuletea picha za Hotel Des Mille Collines (Hotel Rwanda) kama wengi wajuavyo kutoka katika ile muvi, nilikua huku mdau mwenzenu kuhudhuria Tamasha la Pili la Filamu huku Rwanda (Amani Great Lakes Film Festival) ambalo linamalizika leo.

Katika muvi ya Hotel Rwanda watu wanaweza wakaamini kuwa filamu hiyo imefanywa hapa ila ukweli ni kuwa wajamaa (Wamarekani) walikataliwa kuifanya hapa na hivyo walipiga picha hotel na wakaifanyia muvi hiyo Marekani kwahiyo kila kitu katika muvi hiyo ni cha kutengeneza na hotel ndio hiyo katika taswira hizo. Pia ni ukweli vitu vizungumziwavyo katika muvi hiyo juu ya hotel hiyo vilitokea kweli kabisa.

Hoteli hiyo kwa nje
Pia picha nyingine inaonesha tulipokuwa katika mkutano na vijana wanaochipukia katika sanaa ya filamu kutoka Afrika Mashariki na Kati, Kwa mbali kushoto utamuona mwanamke (Karole Karemera) ambaye amecheza kama muhusika mkuu wa kike katika muvi ya 'Sometimes in April' ambayo kila kitu kimefanyika Rwanda.

Wadau wa filamu hapo Bongo nadhani mtaanza kuamka na kufanya mikutano ya maana kwa wadau na washika dau wa filamu nchini ili kuwasaidia wale wanaochipukia na pia kuelimishana juu ya kiwanda kizima cha filamu na sio kukalia mimi flani nimefanya kitu flani, wengine tunawaona tu ila tunaamini hamjui mfanyacho.

Naomba kuwasilisha Mh.Balozi (Usiyekuwa recharble Kigali, Rwanda)


Mdau Dean
Kigali


milioni moja ya zain yaenda karatu

Mfanyakazi wa Zain Tanzania, Ramadhan Hassan akibonyeza kitufe kwenye kompyuta kumpata mshindi wa sh. milioni 1 wa promosheni ya Endesha Ndoto Yako 2 ya Zain Tanzania, Aloyce Yambi wa Karatu. Kushoto ni Ofisa Uhusiano wa Zain Tanzania, Celine Njuju, Meneja Masoko (Kitengo cha Wateja) wa Zain Tanzania, Kelvin Twissa na kulia ni mkaguzi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Abdallah Kahatu.


salamu za mwaka mpya toka arise beauty supplytwanga kupepeta kwa watani wa jadi mwaka mpya

Bendi ya African Stars maarufu kwa jina la Twanga Pepeta International, inaondoka leo kuelekea mjini Nairobi, Kenya kwa ajili ya onyesho maalum la kuuaga mwaka 2008 na kuukaribisha mwaka 2009.

Jumla ya wanamuziki 25 na viongozi watandoka kwa basi maalum la kukodi (SHUTTLE) tayari kwa onyesho hilo la funga mwaka lililoandaliwa na Safari Park Hotel ya mjini Nairobi.
Mwaliko hu unatokana na jinsi Twanga Pepeta ilivyoweza kujikusanyia wapenzi wengi mjini Nairobi na vitongoji vyake na kuwa bendi ya kwanza kupata mialiko mingi nchini Kenya kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati.

Ikumbukwe kuwa hii ni mara ya tano kwa Twanga Pepeta kutumbuiza Kenya ambapo mara ya kwanza ilikua wakati wa uzinduzi maalum wa vituo vya huduma ya tiba, mara ya pili ilikua kwa ajli ya kusheherekea sikukuu ya Wafanyakazi Duniani, Mei Mosi, mara ya tatu ilikuwa ya kuadhimisha miaka ishirini ya “AERC” Taasisi ya Kimataifa inayoo jishughulisha na tafiti za Uchumi na mara ya nne kwa ajili ya uzinduzi wa mtandao wa simu wa Orange.

Kutokana na hilo, Twanga imejijengea umaarufu mkubwa nchin KENYA. Wanamuziki wamejiandaa vilivyo na nyimbo mbali mbali mpya kama “Sumu ya Mapenzi, Nazi Haivunji Jiwe na Mwana Dar es Salaam ambazo zitawekwa hadharani kwa mashabiki wao wa huko Nairobi siku hiyo ya Desemba 31.

Pia nyimbo za zamani kama Safari 2005, Kuolewa, Fainali Uzeeni, Aminata na nyinginezo nyingi zitapigwa siku hiyo kuwapa wapenzi wa burudani ya funga mwaka na kuukaribisha mwaka mpya.

Pia rap mpya kama za Obama, Wizi Mtupu, Kisigino na Kutapika zitatambulishwa kwa mara ya kwanza katika onyeshonyesho hilo ambalo linatarajiwa kuwa la aina yake.

Baada ya onyesho hilo katika mkesha wa mwaka mpya mjini Nairobi Januari Mosi 2009, Twanga itafana nyesho lingine kwenye ukumbi wa Triple A mjini Arusha watakapokuwa wanarejea nchini na siku nayofuata Ijumaa tarehe mbili watatumbuiza Meeda Garden ya Sinza, Mori na Jumamosi Januari 3 watarejea kwenye ngome yao, Mango Garden, Kinondoni na Jumapili mchana watakuwa Leaders Club na usiku, TCC, Chang’ombe.
Hassan Rehani
Meneja


salamu toka ifakara

Halow Michu…
Leo nimekuletea yaliyojiri wakati wa vekesheni yangu mkoani morogoro mji kasoro bahari na kukuletea ya pande hizo. Pichani utaona kivuko cha Mto kilombero na bei za uvushaji. Picha zingine ni moja ya pahala pataaamu na murua pa kujiburudisha panaitwa Mbega resort, huwezi amini ipo ifakara na mpk ukumbi wa mikutano ndani.
Nakutakia siku njema kaka, endeleza libeneke.
Rgards,
John Mnamba.

feri ya ifakara
mbega resort ifakara
AFRICAN LYON

African Lyon FC, formerly Mbagala Market raring to go...

If it wasn't for the love of football of a common Tanzanian, African Lyon Football Club would never have been born.

When vendors of Mbagala Market saw that their region was not represented at the top flight, and there was abundant talent in the area, which was being siphoned by other regional super powers, the vendors decided it was time they saw their kids grow up and challenge the best of the country.

With little or no support, under Jamal Kisongo Mbagala Market was formed from what was a part time social team into a competitive team, which quickly grew in the minds of residents of Mbagala, which is the most populated suburb of the commercial capital of Tanzania, Dar.

Mbagala Market kept growing in popularity, and socially became a household name, of which Mbagla residents were proud of, beating the best teams in it’s division, giving a sigh of relief that infact it was possible for unknown stars to make an impact.

Commitment and forward thinking was the way forward, for the team loved by the common man of Mbagala, which extended it’s wings over the south of Dar Es Salaam, uniting Temeke and southerners from Kigamboni into becoming the team from three suburbs, Temeke, Mbagala and Temeke (TMK).

Having failed to qualify for the top flight on two occasions by a single point, the teams stature outgrew it’s owners and members who decided it was time they got a serious investor, who can only take the team forward.
Having accepted that it was becoming difficult under the circumstances to run the club on donations from the vendors, the team was taken over by a formidable partnership of Vipul Kakad and Shabaan Nyaa who were employees of METL Group of Companies.

The partners have vast experience in club matters, as the METL Group had appointed them to look over sponsorship affairs when METL group was sponsoring top flight Simba sports club in the countries most successful sponsorship package.

Having the support of METL Group CEO Hon. Mohammed Dewji (MP), and company’s sponsorship Mbagala Market transformation was dawning.

Mbagala Market changed it’s name to a more professional name and AFRICAN LYON was born on 10th November, 2008, under the stewardship of Vipul Kakad and Shabaan Nyaa, who received support from the vendors to the old leadership of Jamal Kisongo in competing in the First Division and finishing the first group stage unbeaten.

The priority is now to represent the Mbagala residents in the top flight for the first time since independence, and then to challenge the regional and continental accolades.

African Lyon promises to be a modern administered club, a first for Tanzania, with goals of remaining a fierce competitor of the pitch, upholding social responsibilities, sportsman’s spirit.


hafla ya kuitangaza bongo japan yafana

Mgeni Mh. Balozi Elly E. Mtango akitoa nasaha zake wakati wa hafla hiyo
Hellow Mr Michuzi ,
Hivi majuzi tulikuwa na sherehe ndogo ya kuitangaza Tanzania katika jiji letu la Osaka , shughuli hii iliandaliwa na Ubalozi wetu mdogo wa hapa Osaka kwa mara ya sita mfululizo . Mgeni rasmi alikuwa Mh. E .E.E Mtango ambaye alikaribishwa na President Konoike of Konoike Construction Company kutoa nasaha chache.

Wageni mbali mbali walikuwepo , Mabalozi waliowahi kufanya kazi Africa , wawakilishi toka Osaka City council , viongozi wa Kyocera Comp. , wawekezaji ,wafanyabiashara mbali mbali na fans of Tanzania walikuwepo pia.
Shughuli hii ilifana sana kwa kutumbuizwa na kikundi cha ngoma toka Osaka University na vyakula vya kitanzania kutoka kule nyumbani.

Mengi mazuri yalisemwa , Kyocera waliweza kutoa ahadi ya Solar Panel System 5 kwa ajili ya shule za sekondari , baadhi ya NGOs waliahidi kujenga madarasa ya shule huko nyumbani.
Mark Mrutu
Osaka , Japan
Rais Konoike wa Konoike Construction Company akihtubia
vijana wa kijepu waliowahi kufanya kazi bongo wakitumbuiza kwa nyimbo za kiasili za kibongo

mkwaju ngoma ukirindima

wageni wakitosti kwa furaha

Mh. Balozi Elly Mtango akiwa na wadau
KKKT Mtoni mtongani watoa vyandarua hospitali temeke

Mchungaji wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) usharika wa Mtoni Mtongani Leah Mwankenja akimkabidhi moja ya vyandarua 100 Hidaya Utawangu ambaye ni Afisa Muuguzi wa hospitali ya wilaya ya Temeke kwa ajili ya kutumika katika wodi za hospitali hiyo huku waumini wa kanisa hilo wakishuhudia
Hidaya Utawangu ambaye ni Afisa Muuguzi wa hospitali ya wilaya ya Temeke akivihesabu vyandarua 100 walivyopewa na waumini wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) usharika wa Mtoni Mtongani baada ya kuwapatia vyandarua 100 kwa ajili ya kutumika katika wodi za hospitali hiyo . Picha na Anna Nkinda - Maelezo


Mabingwa wa Tusker Cup 2008 mtibwa football club

mabingwa wa kombe la Tusker 2008 mtibwa fc katika picha rasmi
,


mada jadidu ya bidhaa feki

Kaka Michuzi,
Nimeona hii habari kwenye Daily News kwamba Tanzania imepata hasara ya SHS TRILLIONI 4, (4,000,000,000,000.00). kutokana na BIDHAA FEKI - Link
http://dailynews.habarileo.co.tz/columnist/index.php?id=9185
Jamani kwanini TUENDELEE KUFA NA TUZIDI KUWA MASKINI KWA BIDHAA FEKI?

Kwanini serikali inashindwa kutoa adhabu kali ya kifungo, kufunga biashara permanently na faini kwa wafanyabiashara wanaokutwa na hizi bidhaa? Kuna nchi nyingine wanajadili hukumu ya kifo kwa watu kama hawa.

Hawa ni wauaji kwa sababu,
1) mtu anaumwa malaria yupo hoi halafu anapata dawa feki ya malaria anakufa
2) kuunguza moto nyumba kwa bidhaa feki za umeme na kuua watu na watoto,
3) watu kuumwa magonjwa kutokana na madawa makali na material fake yanayotumika kwa vitu kama rangi za nyumba, malighafi kwa vitu kama redio, maziwa ya watoto, vyakula etc.
4) gari kupata ajali kwa brake pad feki au spare feki. na kuua.

Cha kushangaza bei hazipishani sana kati ya genuine na fake na athari za fake ni kubwa sana.
Serikali ikikamata wafanyabiashara 20 tu na wakapata miaka 20 jela, kila mfanyabiashara aliyekuwa anauza bidhaa feki atafikiria mara mbili kabla ya kuuza, naomba bunge lipitishe muswada wa sheria ya adhabu kali haraka iwezekanavyo na PCB, polisi kwa kushirikiana na Confederation of Tanzania Industries (CTI) vifanye zoezi la kimya kimya, mitaa ya hawa wafanyabiashara inajulikana, uhuru, mnazi mmoja, clock tower etc.

Kuna mambo yanayohitaji misaada na know how kutoka nje lakini hili halihitaji tuna uwezo nalo, kamata bidhaa, tuma sample kwa kampuni mama au mwakilishi wake tanzania fake au siyo feki habari imekwisha.

Mafisadi hawataifurahia hii habari kwa kuwa itawaumiza mirija yao.
WADAU HII MNAIONA IMEKAAJE?
MDAU


kp leomwaka unaagwa kwa dala

mboni mwaka unaisha kwa rahaaaaa. hapa nipo na wadau wenza wa bwawa la maini nyumba ya sanaa baada ya kuangalia mtu analambwa dala. stori kamili nenda BBC kwa kubofya hapa
SALAAM KUTOKA HARBIN, UCHINA

Hi! Kaka Michuzi,
Wakati Dar mnasherehekea sikuu ya xmas kwa kulikabili joto wadau wako tulioko Harbin Uchina tuliamua kushehereka kwa kuutembelea mji wa muda hapa kasikazini mashariki mwa China katika mji wenye baridi sana wa Harbin ambako wameandaa mji wa muda ambao umetengenezwa kwa barafu. Inategemewa huu mji kuishi kwa miezi kama mitatu tu hivi. Kaka wakati sie tunaandaa SABASABA kwa ajili ya maonyesho wenzetu wakati wao unapofika hujenga nyumba na kutengeza mitaa mingi na mizuri yenye urembo wa kila aina kwa kutumia maji (barafu/ice). Mlango wa kuingia msikitini

Waweza kuona wanavyotengeza nguzo na hiyo arch kwa barafu


Wazee wa feki hupendelea sana decorations na hiyo ilikutwa kwenye mtaa wa barafu.

Mjengo huo ni maji (ice) tu hapo